Friday, December 5, 2008

Mapenzi Ya Neema

Wala sistahili
Kuwa hapa mbele zako mpenzi
Wala sistahili
Kuwa mbele ya huu utakatifu

Ni mangapi nimefanya
Ambayo kweli yakuumiza roho
Ni mara ngapi nimekuwa
Nacheza cheza tu na moyo wako

Kwani ni nini nikifanyacho
Kinachokufanya tu unipende
Kwani mimi ningekuwa wewe
Ningenyanyuka nisepe – niende!!

Wala si – stahili – mimi si – stahili
Mapenzi yako yananizidi
Wala si – stahili
Pendo lako lanijaza
Lakini...

Wala sistahili
Kuwa hapa mbele zako Yesu
Wala sistahili
Kusimama mbele ya huu utakatifu


>>to Jesus - the life of my LOVE!!

No comments: